Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zinazo zozana eneo la Sahel zatakiwa kupata suluhu

Pande zinazo zozana eneo la Sahel zatakiwa kupata suluhu

Pande zinazozozana kwenye eneo la Sahara Magharibi zimeonywa kuwa ikiwa hazipata suluhu kwa mzozo wa kisiasa unaoendelea huenda tena kukawa na dhuluma za kijeshi. Mapigano yalilipuka katika eneo la Sahara Magharibi kati ya Morocco na eneo la Polisario mwaka 1976 baada ya kuondoka kwa utawala wa kikoloni wa Hispania.

Morocco inataka eneo hilo kutangazwa huru huku eneo la Polisario likiunga mkono kufanyika kwa kura ya maoni. Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Sahara Magharibi Christopher Ross anasema kuwa ikiwa suluhu halitapatikana huenda kukawa na madhara makubwa.

(SAUTI YA CHRISTOPHER ROSS)