Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa AIEA kuzuru Iran wiki ijayo

Wataalamu wa AIEA kuzuru Iran wiki ijayo

Wataalamu kutoka shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA watazuru Iran wiki ijayo katika juhudi za kutatua masuala yaliyopo kuhusiana na mipango ya nyuklia ya nchi hiyo.

Hatua ya kutuma wataalamu Iran imetangazwa leo Jumatatu na IAEA na shirika hilo limesema kuna taarifa za kuaminika kwamba Iran inaunda silaha za nyuklia na limeitaka serikali kuafiki ziara ya timu ya IAEA ili kutanabaisha mfumo wa mipango hiyo ya nyuklia

Katika taarifa hiyo ya IAEA iliyotolewa mjini Vienna makao makuu ya shirika hilo mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano ametangaza kwamba ziara hiyo itafanyika kuanzia Januari 29 hadi 31.

Timu hiyo itaongozwa na mkurugenzi wa usalama Herman Nackaerts na itajumisha pia mkurugenzi wa sera wa shirika hilo Rafael Grossi.

Iran imesisitiza mara kadhaa kwamba mipango yake ya nyuklia ni ya amani na ni ya kutoa nishati kwa watu wake, lakini nchi nyingi zinadhani kuwa inaunda silaha za nyuklia.