Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani kushambuliwa mkutano wa chama kilichokuwa tawala Ivory Coast

UM walaani kushambuliwa mkutano wa chama kilichokuwa tawala Ivory Coast

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha operesheni ya amani nchini Ivory Coast UNOCI vimelaani vikali tukio la shambulizi lililofanywa katika mkusanyiko uliwajumuisha wafuasi na wanchama chama kilichokuwa tawala nchini humo, waliokusanyika Mjini Abidjan mwishoni mwa wiki.

Chama hicho Ivorian Popupalar Front, kilichokuwa madarakani kwenye utawala uliopita, kilikuwa kikiendesha mkutano wake wa hadharani lakini mkutano huo uliingia dosari baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Katika tukio hilo watu kadhaa walijerihiwa lakini hakuna ripoti juu ya watu kupoteza maisha.

Ikilaani vikali tukio hilo, Umoja wa Mataifa imetaka kuwepo kwa hali ya utulivu na imevitaka vyama vya siasa kujiepusha na jazba zinazoweza kuchochea hali mbaya ziadi ya kisiasa.