Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washtakiwa wanne wa Kenya waahidi kupambana na uamuzi wa ICC

Washtakiwa wanne wa Kenya waahidi kupambana na uamuzi wa ICC

Baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kutangaza uamuzi wake dhidi ya washitakiwa wanne wa makosa yatakayowakabili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu wameahidi kapambana na uamuzi huo wa mahakama. William Ruto amesema mawakili wake wako tayari kukata rufaa na kukabiliana na uamuzi huo.

(SAUTI YA WILLIAM RUTO)

Mwandishi wa habari Joshua Sanga kwa upande wake amesema hakutarajia na anapinga uamuzi huo.

(SAUTI YA JOSHUA SANG)

Naye Rais wa Kenya Mwai Kibaki amesema amemuamuru mkuu wa sheria Kenya kuteuwa kundi la wanasheria watakaoshauri ipasavyo dhidi ya uamuzi huo wa ICC.

(SAUTI YA RAIS MWAI KIBAKI)

Jumanne Januari 24 mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo atafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia uamuazi wa ICC dhidi ya washitakiwa hao wanne.