Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusini na Mashariki mwa Afrika ndio waathirika wakubwa wa HIV:UNAIDS

Kusini na Mashariki mwa Afrika ndio waathirika wakubwa wa HIV:UNAIDS

Hatua zaidi zinahitajika ili kupunguza maambukizi mapya ya HIV Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika amesema Dr Sheila Tlau mkurugenzi wa kanda ya mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS.

Dr. Tlau amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva leo kwamba robo tatu ya watu milioni 34 wanaoishi na virsi vya HIV duniani wako Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Amesema hata hivyo kanda hiyo imepiga hatua kupunguza maambukizi mapya. Ameongeza kuwa kati ya mwaka 1997 hadi sasa wamepunguza maambukizi mapya kwa asilimia 25-26, hata hivyo bado yanashuhudiwa maambukizi mapya katika baadhi ya nchi.