Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadilio ya mawasiliano kwa njia ya masafa huenda kukaathiri utabiri wa mabadiliko ya hali ya hewa

Mabadilio ya mawasiliano kwa njia ya masafa huenda kukaathiri utabiri wa mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO  linasema kuwa watabiri wa hali ya hewa , wanaotoa onyo la majanga na wachunguzi wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa wanategemea masafa yanayotumika masaa ishirini na manne. Hata hivyo mabadiliko katika matumizi ya masafa ya Radio huenda yakaaathiri jitihada za kuelewa na kutabiri mabadiliko ya hali ya hewa. Mikutano iliyofanyika awali kuhusu mawasilino kupitia masafa ya Radio yamelipa kipaumbele suala la kulinda masafa yanayopatikana katika utabiri wa hali ya hewa huku mkutano unaokuja ukitarajiwa kuchukua mkondo huu.