Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama latiwa hofu na hali inayoendelea Jonglei

Baraza la Usalama latiwa hofu na hali inayoendelea Jonglei

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani kupotea kwa maisha ya watu, kuathirika kwa maisha ya maelfu kutokana na machafuko kwenye jimbo la Jonglei Sudan Kusini.

Katika taarifa waliyoitoa Jumatatu usiku wajumbe hao wa Baraza la Usalama wamesisitiza kuhusu jukumu muhimu la serikali ya Sudan Kusini ambalo ni kuwalinda raia wake na hususani makundi ya wasiojiweza kama wanawake na watoto. Wajumbe hao wamerejea wito kwamba ghasia na machafuko ya aina yoyote ile hayakubaliki na wamezitaka jamii zote za Jonglei kumaliza mzunguko wa machafuko mara moja na kujihusisha na mchakato wa amani kwa njia ya upatanisho.