Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asitushwa na kifo cha Rais wa Guinea-Bissau

Ban asitushwa na kifo cha Rais wa Guinea-Bissau

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa na kushitushwa na kifo cha Rais Malam Bacai Sanha kilichotokea leo mjini Paris Ufaransa.

Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Rais Sanha na watu wote wa Guinea-Bissau kwa msiba huo mkubwa. Ameongeza kuwa Sanha alikuwa kiongozi shupavu aliyeiongoza nchi hiyo katika kipindi kigumu cha historia yake. Na amesema anaamini mipango iliyoainishwa na katika ya nchi hiyo katika kumpata mrithi wa Rais Sanha itaheshimiwa na kufuata na amewahahakikishia watu wa Guinea-Bissau na serikali yao kuwa wataendelea kupata msaada wa Umoja wa Mataifa. Joao Soares da Gama ni balozi wa Guinea-Bissau kwenye Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA JOAO SOARES DA GAMA)