Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Ugiriki na Uturuki wakutana Nicosia

Viongozi wa Ugiriki na Uturuki wakutana Nicosia

Viongozi wa jamii ya Cyprus ya upande wa Uturuki na Ugiriki wanakutana Nicosia Jumatatu hii kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kuunganisha kisiwa cha Cyprus.

Cyprus imegawanyika baina ya jamii mbili tangu mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na kundi linalopendelea muungano na Ugiriki na kuifanya Uturuki kutuma vikosi katika kisiwa hicho. Vikosi hivyo vikaweka udhibiti wa Cyprus ya Uturuki dhidi ya eneo la kaskazini la kisiwa hicho.

Umoja wa Mataifa unawezesha mazungumzo hayo baina ya viongozi wa jamii hizo mbili ili kuunda serikali ya Cyprus ya Ugiriki na Cyprus ya Uturuki zenye hadhi sawa.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa miaka kadhaa sasa kwa makatibu wakuu mbalimbali wakijaribu kuzisaidia jamii hizo kupata suluhu ya mvutano.