Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka suluhu ya mezani kutanzua hali mbaya ya kisiasa Iraq

UM wataka suluhu ya mezani kutanzua hali mbaya ya kisiasa Iraq

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na meza ya majadiliano ili kutanzua mkwamo wa kisiasa unafukuta nchini Iraq ukisema kuwa hali ya uhasama inayoendelea sasa haiwezi kutatuliwa kwa kupuuzia majadiliano.

Martin Kobler ambaye ni mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu kwenye eneo hilo amesema kuwa mwishoni mwa wiki amekutana na bunge la Iraq na kulitolea mwito namna linavyopaswa kushughulia mzozo wa eneo hilo kwa majadiliano ya mezani.

Ametaka pande zote kujongelea meza ya majadiliano kwani ndiyo shabaha inayoweza kulivusha taifa hilo hasa katika kipindi hiki ambacho vikosi vya kigeni ninaondoka nchini humo.

Amewataka pia wanasiasa wa Iraq pamoja na makundi mengine kuhakikisha kuwa hayaendelea kuvuga ustawi wa taifa hilo.