Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya amani Israel-Palestina vyatajwa:UM

Vikwazo vya amani Israel-Palestina vyatajwa:UM

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye mazungumzo ya usakaji amani mashariki ya kati amesema kuwa amevunjika moyo na namna pande zinazohusika kwenye mazungumzo hayo zinavyoshindwa kuondoa tofauti zao.

Amesema hatua ya Israel kuendelea na ujenzi wa makazi ya walowezi ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha juhudi za kutanzua mzozo huo. Bwana Robert Serry amedai kwamba kungekuwa ni jambo la kutia moyo kukaribisha mwaka mpya kwa matumaini iwapo Israel ikingesitisha mpango wake wa ujenzi wa makazi ya walowezi kwenye eneo la Palestina.

Palestina imesisitiza kuwa haitakuwa tayari kurejea tena kwenye mazungumzo ya moja kwa moja ya usakaji amani iwapo Israel haitasitisha kwanza mpango wake huo.