Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapiga hatua ya kukabiliana na Ukimwi kwa mwaka wa 2011

UM wapiga hatua ya kukabiliana na Ukimwi kwa mwaka wa 2011

Mwaka 2011 umetajwa kama mwaka wa mabadiliko hasa kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi. Suala la ukimwi limekuwa likionekana kuwa changamoto kubwa lakini sayansi, mchango wa kisiasa na kujitolea kwa jamii vimesababisha kuwepo kwa mafanikio katika vita dhidi ya ukimwi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limesema kufikia lengo la sufuri ndio ilikuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya ukimwi duniani inayoidhinishwa Desemba mosi. Kauli mbiu hii itatumika hadi mwaka 2015 na kuchagiza mtazamo wa UNAIDS pamoja na WHO wa kufikia maambukizi mapya sufuri, unyanyapaa sufuri na vifo vitokanavyo na ukimwi sufuri na kusema kila. Mashirika haya yamesema kila mtu katika jamii zote duniani ana fursa ya kuchangia ili kuweze kuwa na mafanikio katika lengo hili.

(MAONI)