Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi waendelea kukimbia makwao Sudan Kusini

Watu zaidi waendelea kukimbia makwao Sudan Kusini

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo pia ya kitaifa na kimataifa yanaendelea kuwasadia watu waliokimbia makwao kufuatia kuwepo uvamizi kwenye jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini. Zaidi ya watu 7000 waliokimbia makwao kutoka kaunti za Twic East na Bor kwa sasa wamewasili kwenye kaunti ya Bor.

Waliohama makwao wengi wakiwa ni wanawake, watoto na watu wazee wanaishi kwenye makao ya tume ya kutoa huduma za dharura. Kati ya misaada ya chakula waliyopewa wakimbizi hao ni pamoja maharagwe, mafuta ya mboga na chumvi pamoja na misaada isiyokuwa chakula kama mablanketi sahani na neti za mbu.