Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Banki ya dunia kufadhili huduma za afya kwa Watanzania milioni 8 kila mwaka

Banki ya dunia kufadhili huduma za afya kwa Watanzania milioni 8 kila mwaka

Watanzania takribani milioni 8 watakuwa na huduma bora za afya kila mwaka kuanzia sasa hadi mwaka 2015 kufuatia hatua ya Benki ya dunia kuidhinisha dola milioni 100 kwa ajili ya mradi ya huduma muhimu za afya nchini humo.

Mradi huo mpya umeandaliwa kuendeleza mafanikio ya Tanzania ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ambazo zimesaidia kupunguza idadi ya vifo vya watoto kwa karibu nusu katika muongo uliopita.

Kwa mujibu wa Mercy Tembon kaimu mkurugenzi wa benki ya dunia nchini Tanzania, lengo la milenia la kupunguza idadi ya vifo vya watoto ifikapo mwaka 2015 iko ndani ya uwezo wa Tanzania. Na kwamba watoto wa Tanzania leo wana fursa kubwa ya kuishi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita nchini humo.