Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa hofu na matukio ya kiusalama kwenye kambi ya Dadaab

UNHCR yatiwa hofu na matukio ya kiusalama kwenye kambi ya Dadaab

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limetiwa hofu na matukio ya karibuni ya kiusalama kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko Kaskazini mwa Kenya. Dadaab ni kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani ikihifadhi watu zaidi ya 460,000.

Kwa mujibu wa shirika hilo mlipuko wa Jumatatu uliua mtu mmoja na kujeruhi maafisa wawili wa polisi kambini hapo. Huku mlipuko mwingine ukitokea Jumanne karibu na soko kwenye kambi ya Ifo na kuharibu gari la polisi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)