Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakaribisha hatua ya Israel kuwaachilia wafungwa watoto wa Palestina

UNICEF yakaribisha hatua ya Israel kuwaachilia wafungwa watoto wa Palestina

Umoja wa Mataifa umekaribisha kuachiliwa huru kwa watoto 55 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa na Israel ikiwa sehemu ya mpango kwa pande hizo mbili kubadilishana wafungwa mpango ulioasisiwa miezi miwili iliyopita.

Hata hivyo shirika la kuhudumia watoto UNICEF limesema kuwa linategemea kuona hatua zaudi zikipigwa katika siku za usoni.

Hii ni maraa ya pili kuachiliwa kwa wafungwa kwa pande zote, na mara ya kwanza ilikuwa Octoba 18 wakati kundi la Hamsi lilipomwachia askari wa Israel Gilad Shalit ambaye alikuwa akishikiliwa Palestine tangu June 2006.

Kuachia huru kwa askari huyo kulifungua mlango kwa wafungwa wengine 477 wa Kipalestina ambao walizuiliwa kwenye magereza ya Israel.