Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya pamoja kwa ajili ya amani Darfur yazinduliwa:Gambari

Tume ya pamoja kwa ajili ya amani Darfur yazinduliwa:Gambari

Juhudi za kuleta amani ya kudumu kwenye jimbo la Darfur Sudan zimepiga hatua nyingine Jumapili kwa kuzinduliwa tume ya pamoja JC ambayo ni taasisi muhimu itakayohakikisha utekelezaji wa makubaliano ya mwisho ya usalama yaliyoafikiwa Doha Qatar.

Mkutano wa uzinduzi huo umefanyika mjini Khartoum na Ibrahim Gambari ambaye ni mkuu wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani Darfur UNAMID, na pia mpatanishi mkuu wa muda Darfur amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa lazima isaidie pande husika katika muafaka huo na isipoteze matumaini ya watu wa Darfur ya kupata amani ya kudumu na maendeleo

(SAUTI YA IBRAHIM GAMBARI)

Miongoni mwa majukumu mengine ya JC ni kutatua mivutano baina ya pande husika na kutafsisri mkataba wa kusitisha vita na mipango ya mwisho ya usalama. Gambari amesema pia mapigano ya kijeshi yamepungua Darfur ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya UNAMID na walinda amani wengine katika baadhi ya sehemu.