Jamii ya kimataifa yatakiwa kupinga dhuluma dhidi ya wanawake

Jamii ya kimataifa yatakiwa kupinga dhuluma dhidi ya wanawake

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo ameishauri jamii ya Umoja wa Mataifa na washika dau wengine kushughulikia zaidi mahitaji ya watu wa Somalia yakiwemo masuala ya kibinadamu na haki za wanawake.

Bi Manjoo amesisitiza kuwa hata kama kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa ili kufadhili huduma za kibinadamu nchini Somalia bado maisha ya wasomali wa kawaida hajaimarika huku maelfu wakiwa bado wakiwa wanaishi maisha magumu. Monica Morara na taarifa kamili.