Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua kampeni ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu Mogadishu

UM wazindua kampeni ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu Mogadishu

Shirika la afya duniani WHO limezindua kampeni ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu mjini Mogadishu nchini Somalia hii leo kampeni ambayo ni yenye lengo la kutoa hamasisho kuhusu maradhi ya kipindundu na ya kuendesha miongoni mwa Wasomali.

Somalia ilikabiliwa na mkurupko mbaya wa ugonjwa wa kipindupindu mwaka 2007 ambapo visa 67,000 viliripotiwa. Hata hivyo kusafishwa kwa maji yanayoingia mjini Mogadishu na jitihaza za kuboresha usafi vimezuia kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo. Lindmeier ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA CHRISTIAN LINDMEIER)