Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utulivu waendelea nchini Haiti

Utulivu waendelea nchini Haiti

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti ameitaja hataua ya kuchaguli kwa rais mpya nchini Haiti mapema mwaka huu kama jambo liloleta udhabiti nchini humo.

Haiti imeshakumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililofuatiwa na mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kati ya kipindi cha miaka miwili ambapo maelfu ya watu waliaga dunia. Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti Mariono Fernandez amesema kuwa kumepigwa hatua lakini hata hivyo kuna changamoto zimesalia.

(SAUTI YA MARIONO FERNANDEZ)