Baraza la Usalama larefusha muda kwa jopo la wataalamu wanafuatilia vikwazo kwa Liberia

15 Disemba 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limerefusha muda kwa jopo la wataalamu linalofuatilia utekelezwaji wa vikwazo vilivyowekewa kwa Liberia, likiweka zingatio jipya juu ya uwezekano wa kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Jopo hilo la wataalamu liliundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon July 2007 kwa shabaha kuangalia upya kama vikwazo vilivyowekwa kwa utawala wa zamani wa Charles Taylor vilizingatiwa ipasavyo ama au la.

Katika uamuzi wake mpya, Baraza la Usalama limeongeza muda kwa jopo hilo kwa kipindi ncha miezi 12.

Kwa kuda huo jopo hilo linatazamiwa kufuatilia kwa karibu pamoja na kufanya tathmini kama kulikuwa na ukiukwaji wa marafuku hiyo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter