Mahakama ya ICTR yampunguzia kifungo afisa mmoja wa zamani

15 Disemba 2011

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu wa kivita iliyobainiwa baada ya kutokea mauaji ya halaiki nchini Rwanda ICTR imepunguza kifungo cha afisa mmoja wa zamani aliyehukumiwa mwaka uliopita kwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ambapo maelfu ya watutsi waliuawa.

Dominique Ntawukulilyayo sasa amepewa kifungo cha miaka 20 badala ya miaka 25 jela baada ya uamuzi ulitolewa na upande wa rufaa wa mahakama ya ICTR.

Wakati wa kesi yake mahakama ilifahamishwa kuwa Bwana Ntawukilyayo aliwashauri watutsi waliokusanyika kwenye soko la Gisagara waElekee kwenye mlima wa Kabuye ambapo watalindwa na kulishwa lakini baadaye alipeleka jeshi na kuwauwa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter