Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Asia-Pacific wajadili maendeleo kwa mataifa maskini kwenye kanda yao:ESCAP

Viongozi wa Asia-Pacific wajadili maendeleo kwa mataifa maskini kwenye kanda yao:ESCAP

Wataalamu na maafisa wa mataifa ya Asia-Pacific wanasema licha ya hatua zilizopigwa katika miaka kumi iliyopita mataifa masikini na visiwa vidogo vinavyoendelea wamesalia kuwa wahanga wa matatizo ya kichumi na majanga mengine ya ndani na nje katika kanda huo.

Wamesema msukosuko wa kiuchumi duniani na changamoto zingine kama kuongezeka kwa matatizo ya chakula, upungufu wa nishati, kupanda kwa bei za bidhaa na matatizo ya fedha duniani yamebadili mfumo wa hatua za maendeleo katika mataifa hayo masikini ambazo zilipigwa katika miaka kadhaa ya nyuma. Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii kwa mataifa ya Asia-Pacific ESCAP Shun-ichi Murata aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano mjini Bankok Thailand wadau wote wa lazima wajadili njia za kushughulikia hali ya kutokuwepo kwa usawa hasa wa maendeleo katika eneo la Asia-Pacific.