Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuapishwa kwa serikali mpya nchini Yemen

Ban akaribisha kuapishwa kwa serikali mpya nchini Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribishwa kuapishwa kwa serikali ya umoja nchini Yemen akiitaja kama hatua muhimu ya utekelezwaji wa mabadiliko nchini humo.

Ban ameupongeza uongozi wa makamu wa rais Hadi waziri mkuu Basandwa na pande zilizohusika katika kuibuni serikali wakati ufaao kuambata na makubalino yaliyotiwa sahihi mjini Riyadh Novemba 23.

Chini ya makubaliano hayo rais Ali Abdullah Saleh alikubali kuachilia madaraka kwa makamu wa rais Abed Rabbo Mansour al-Hadi huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kuandaliwa kwa muda wa miezi mitatu ijayo.