Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi na magonjwa ya zinaa wakamilika Addis Ababa

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi na magonjwa ya zinaa wakamilika Addis Ababa

 

Mkutano wa 16 wa kimataifa kuhusu ukimwi na magonjwa ya zinanaa barani Afrika (ICASA) kwa mwaka 2011 umehitimishwa Alhamisi mjini Addis Ababa Ethiopia. Mkutano huo mkubwa kabisa wa ukimwi barani Afrika umewaleta pamoja washiriki zaidi ya 10,000 kutoka nchi 103 duniani wakiwemo wanasayansi, wahudumu wa afya, watu wanaoishi na virusi vya HIV, watunga sera, jumuiya za kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali, wanaharakati na wawakilishi wa serikali.

Ajenda kuu zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kujifunza na kubadilishana zoefu, mafanikio na kuzungumzia changamoto na ubunifu katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya HIV na ukimwi barani Afrika.