Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiongozi wa zamani wa Khmer Rouge akanusha madai ya kuhusika kwenye mauwaji ya Cambodia

Kiongozi wa zamani wa Khmer Rouge akanusha madai ya kuhusika kwenye mauwaji ya Cambodia

Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Kikomonist katika eneo la Kampuchea Nuon Chea, ameyakana mashtaka dhidi yake juu ya uendeaji kinyume wa haki za binadamu na mauwai ya watu, matukio yanayodaiwa kutendeka wakati wa utawala wa mkono wa Khmer Rouge katika kipindi cha kuanzia mwaka 1975 hadi 1979 huko Cambodia.

Akipanda kizimbani kwa mara ya kwanza kuyakabili mashtaka dhidi ya uhalifu wa binadamu, kiongozi huyo wa zamani amesema kuwa hatambui kufanyika kwa mauwaji hayo, lakini anachojua yeye ni kuwa watu wa Vietnam ndiyo waliotekeleza mauwaji hayo na wala siyo yeye wala watu wa Cambodia.

Mbele ya jopo la wataalamu wanaosikiliza kesi hiyo huko Phnom Penh mtuhumiwa huyo amesisitiza kuwa yeye ni mtu safi na wala mikono yake hainuki damu. Yeye pamoja na waliokuwa maafisa wengine wa kundi hilo la Khmer Rouge wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama maalumu ya kimataifa ya uihalifu wa kivita inayotambulika kama ECCC: