Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Vietnam kufunga vituo vya lazima vya watumiaji wa mihadarati na makahaba

UM waitaka Vietnam kufunga vituo vya lazima vya watumiaji wa mihadarati na makahaba

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya afya Anand Grover amehitimisha ziara yake nchini Viet Nam Jumatatu na kusisitiza kwamba mahabusu na vituo vya lazima vya matibabu kwa watumiaji wa mihadarati na makahaba vinakiuka haki za watu hao za afya.

Bwana Grover amesema watu hao wananyimwa haki yao ya kuwa huru na matibabu ya kutojiamulia na pia haki ya kutopewa taarifa na kukubali kwa hiyari masuala yote yanayohsiana na maamuzi ya matibabu kwao. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)