UNAIDS yapongeza uamuzi wa China kuziba pengo lake katika vita vya Ukimwi

1 Disemba 2011

Serikali ya Uchina imetoa wito wa kushirikiana kubeba jukumu la kufikia lengo la maambukizi mapya ya HIV sufuri, unyanyapaa sufuri na vifo sufuri vitokanavyo na ukimwi. Pia imeahidi kuziba pengo lake la fedha za kupambana na ukimwi kwa kuongeza uwekezaji wa ndani.

Ahadi hiyo imetolewa katika maadhimisho ya siku ya ukimwi na waziri mkuu wa China Wen Jiabao mjini Beijing na kupongezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS. Hata hivyo China imesema pamoja na tangazo hilo msaada wa mfuko wa kimataifa yaani Global Fund bado utahitajika nchini humo.

Nao wananchi wa Afrika wanasemaje kuhusu siku hii ya ukimwi duniani?

(MAONI YA SIKU YA UKIMWI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter