Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaitaka Belarus kuwaachilia wafungwa wa kisiasa

29 Novemba 2011

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imerejelea wito wake kwa serikali ya Belarus wa kuitaka iwaachilie huru wapinzani wote wa kisiasa, wanaharakati na waaandishi wa habari waliofungwa kwa kutekeleza haki zao na kukomesha hatua ambazo zinalenga kuwahangaisha watetesi wa haki za binadamu.

Kwenye taarifa iliyotolewa hii leo ofisi hiyo inasema kuwa kuhukumiwa kwa mtetesi maarufu wa haki za binadamu nchini Belarus Ales Bialtski kifungo cha miaka minne na nusu gerezani ni jambo la kukasirisha na la tisho kwa mashirika ya umma nchini Belarus.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter