Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za dharua za misaada Somalia zaokoa maisha ya watoto

Hatua za dharua za misaada Somalia zaokoa maisha ya watoto

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Matifa UNICEF linasema kuwa kumekuwa na kupungua kwa maeneo yaliyokumbwa na njaa kusini mwa Somalia kutokana na misaada inayotolewa na wafadhili tangu kutangazwa kwa njaa nchini Somalia mwezi Julai.

Mwakilishi wa UNICEF Sikander Khan anasema kuwa maelfu ya watoto wameokolewa. UNICEF inasema kuwa hata baada ya kupungua kwa idadi ya vifo, viwango vya wanaokumbwa na utapiamlo vinasaliwa kuwa vya juu kwenye sehemu nyingi nchini Somalia. Nayo mikurupuko ya magonjwa inayotarajiwa kusababishwa na mvua zinazoonyesha yanahatarisha maisha ya watoto miezi inayokuja. Hadi sasa takriban watu milioni nne wanahitaji misaada ya kuokoa maisha.