Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awapongeza waliberia kwa kuendesha uchaguzi huru na wa haki

Ban awapongeza waliberia kwa kuendesha uchaguzi huru na wa haki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Liberia kwa kutekeleza haki yao ya kupiga kura kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais mapema mwezi huu na kupongeza uongozi wa taifa hilo kwa kuendesha uchaguzi huru, wazi na wa haki.

Lakini amelaani pia ghasia zilizozuka siku moja kabla ya uchaguzi huo uliofanyika Novemba 8. Amekaribisha hatua ya serikali ya kuunda tume huru ya kuchunguza ghasia hiyo. Monica Morara anaripoti.

(RIPOTI YA MONICA MORARA)