Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laani mashambulizi dhidi ya balozi Syria

Baraza la Usalama laani mashambulizi dhidi ya balozi Syria

Baraza la Usalama limeshutumu vikali mashambulizi yaliyozilenga balozi kadhaa nchini Syria na limetaka mamlaka nchini humo kutoziendea kinyume sheria za kimataifa. 

Kwa mujibu wa duru za vyombo vya habari, makundi ya waandamanaji yanayofungamana na serikali, yameshambulio ofisi kadhaa za kibalozi, ikiwemo zile zilizoko katika mji mkuu Damascus na kuharibu majengo kadhaa. 

Mashambulizi hayo yamekuja kufuatia hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu kuitimua Syria kwenye uwanachama wa Jumuiya hiyo huku ikiiwekea vikwazo kadhaa.

Katika taarifa yake, baraza hilo limeshutumu vikali vitendo vya aina hiyo ikisema kuwa vimevuruga utendaji wa shughuli za kidiplomasia.