Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya makao ya balozi nchini Syria

UM walaani mashambulizi ya makao ya balozi nchini Syria

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi kwenye balozi kadha kwenye mji mkuu wa Syria Damascus. Katika siku za hivi majuzi wafuasi wa rais Bashar Al-Assad wameshambulia balozi za Uturuki, Qatar, Saudi Arabia na Ufaransa.

Kwenye taarifa yake kwa mara nyingine baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limerejelea wito wake wa kutaka kulindwa kwa mali za balozi na kuheshimu sheria ya kimataifa. Balozi Jose Filipe Moraes Cabralni rais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

(sauti ya CABRAL)