Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi dhidi ya wanajeshi wa UNAMID Darfur

Ban alaani shambulizi dhidi ya wanajeshi wa UNAMID Darfur

Mwanajeshi mmoja wa kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID, ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia shambulizi lilitekelezwa kwenye mji wa Nyala ulio Darfur Kusini. Shambulizi hilo linajiri mwezi mmoja baada ya walinda amani wengine watatu kuuawa Darfur Kaskazini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulizi hilo na kuitaka serikali ya Sudan kuwachukulia hatua wahusika. Zaidi ya wanajeshi 30 wameuawa tangu UNAMID ichukue usukani kutoka kwa kikosi cha Muungano wa Afrika mwaka 2008 .