Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaelezea ushirikiano kati yake na UM

ICC yaelezea ushirikiano kati yake na UM

Rais wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC amesema kuwa uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Umoja wa Mataifa unaendelea kuwa wenye umuhimu. Akihutubia nchi wanachama wa mahakama hiyo Jaji Sang Hyun Song amesema kuwa kati ya wajibu wa ICC na Umoja wa Mataifa ni pamoja na kuzuia na kuwaadhibu waliotenda uhalifu duniani.

Mahakama ya ICC iliyo na makao yake makuu mjini Hague ndiyo mahakama ya kwanza ya kimataifa iliyobuniwa kuwahukumu wanaohusika kwenye vitendo uhalifu vikiwemo mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.