Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 500,000 hufa kila mwaka kutokana na ghasia zinazohusisha silaha:UM

Zaidi ya watu 500,000 hufa kila mwaka kutokana na ghasia zinazohusisha silaha:UM

Ripoti ya kimataifa ya mzigo utokanao na ghasia za kutumia silaha kwa mwaka 2011 inasema takribani watu 526,000 wanakufa kila mwaka kutokana na ghasia zinazohusiha matumizi ya silaha, ikiwa ni zaidi ya watu 1,400 kila siku.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu wanaokufa katika vita kila mwaka ni 55,000, hii ni ndogo sana ikilinganishwa na makadirio ya 396,000 ya wanaouawa nje ya vita kila mwaka. Watu wengine 54,000 wanakufa kutokana na ghasia za bila kukusudia na mauaji ya bahati mbaya. Keith Krause ni mkurugenzi wa mpango wa utafiti wa silaha ndogondogo.

(SAUTI YA KETH KRAUSE)

Ameongeza kuwa El Salvador ndiyo nchi iliyoathirika sana na uhalifu na ghasia za kutumia silaha ikifuatiwa na Iraq na Jamaica.