Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya yasababisha watu kuhama nchini Somalia

Mapigano mapya yasababisha watu kuhama nchini Somalia

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasisi uliopo kufuatia ghasia zinazoendelea kusini mwa Somalia. Ghasia hizo mpya ni kati ya makundi hasimu suala ambalo limechangia hali iliyopo sasa ya njaa kuwa mbaya zaidi.

Hata hivyo makundi yote yaliyojihami nchini Somalia yametakiwa kukoma kulenga maeneo waliko raia na kuhakikisha kuwa maisha ya raia hayamo hatarini. Kumekuwa na ripoti za vifo na majeraha hata kama bado ripoti zenyewe hazijathibitishwa. Adrian Edward kutoka UNHCR anaeleza

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)