Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Ivory Cost azungumzia majaliwa ya nchi yake

Rais wa Ivory Cost azungumzia majaliwa ya nchi yake

Rais wa Ivory Coast amesema mkwamo wa kisiasa uliojiri Afrika Magharibi, kama  Ivory Coast, nchi ambayo hivi karibuni ilishuhudia machafuko ya kisiasa, amesema kuwa taifa hilo lipo kwenye mkondo salama na halina wasiwasi juu ya majaliwa yake. Rais Alassane Ouattara amewahakikishia viongozi wa dunia wanaokutana New York kwamba upepo mbaya wa kisiasa uliovuma kwenye eneo la Afrika Magharibi hivi sasa hauna nafasi tena.

Amesema kuwa hali mbaya ilijiri nchini mwake wakati wa uchaguzi mkuu ni hekaya za kale ambazo haziwezi kupena nafasi tena na kuongeza kuwa nchi yake imeanza kupiga hatua kusonga mbele. Rais huyo amesema kuwa nchi yake iko tayari kuwakaribisha wafanyabiasha wanataka kwenda kuweka nchini humo.