Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 200,000 huenda wakakabiliwa na janga kwenye jimbo la Kordofan Kusini

Zaidi ya watu 200,000 huenda wakakabiliwa na janga kwenye jimbo la Kordofan Kusini

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa huenda zaidi ya watu 200,000 walioathirika na mapigano ya hivi majuzi kwenye eneo la Kordofan Kusini wakabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo na vifo baada ya serikali ya Sudan kuzuia mashirika ya kutoa misaada kusambaza misaada hiyo.

Mratibu wa masuala ya kibindamu kwenye Umoja wa Matifa Bi Valerie Amos amesema kuwa hali kati eneo hilo imekuwa mbaya sana. Awali Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa habari kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendwa kwenye eneo hilo wakati kunapoendelea mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Sudan na na kundi la Kaskazini la Sudan People’s Liberation Army North. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)