Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia imetakiwa kuonyesha mshikamano zaidi kwa serikali ya mpito ya Somalia:UM

Dunia imetakiwa kuonyesha mshikamano zaidi kwa serikali ya mpito ya Somalia:UM

Mkutano wa maalumu kuhusu Somalia uliohudhuriwa na kuwezeshwa na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia, Balozi Augustine Mahiga, Muungano wa Afrika na wadau wengine umekamilika mjini Moghadishu. Mkutano huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Somalia umetoka na mapendekezo kadhaa ikiwemo pongezi kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwa hatua iliyopiga kwa mipango ya kurejesha usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa balozi Mahiga mkutano huo umetoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia vifaa na kuviwezesha vikosi vya kulinda amani vya Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM ili kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Pia umeshukuru jitihada za serikali ya Japan kusaidia kufufua jeshi la polisi la Somalia, na juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA katika kusaidia Somalia, na wameliomba shirika hilo kufanya mazungumzo na serikali ya mpito kujadili suluhu ya kame na njaa ili kuepuka taifa hilo kuendelea kutegemea misaada.