Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madai ya askari wa UM kusaidia kutorosha madini huko DRC yaanza kuchunguzwa

Madai ya askari wa UM kusaidia kutorosha madini huko DRC yaanza kuchunguzwa

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Congo vimeanza kushirikiana na mamlaka za nchi hiyo ili kuendesha uchunguzi kuhusiana na tuhumu za mfanyakazi mmoja wa vikosi hivyo kujihusisha na vitendo kutorosha madini kwa njia ya panya.

Maafisa wa vikosi hivyo MUNUSCO wamesema kuwa mwajiri mmoja wa vikosi hivyo anadaiwa kuhusika kutorosha tani moja ya madini aina cassiterite na kusafirisha hadi nchi jirani ya Rwanda. Maafisa wa Congo hapo jana walitoa malalamiko wakidai kuwepo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaojihusisha na biashara ya utoroshaji wa madini kwa njia ya magendo. Hata hivyo MUNUSCO imesema kuwa itaendelea kushirikiana na mamlaka za Congo ili kubaini ukweli wa mambo.