Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala wa Sudan wamuachilia mfanyikazi wa UNAMID

Utawala wa Sudan wamuachilia mfanyikazi wa UNAMID

Mfanyikazi mmoja wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID aliyekuwa amezuiliwa ameachilwa huru kutoka kizuizini ikiwa ni karibu miezi mitatu tangu akamatwe. Idriss Abdelrahman, aliachiliwa hii leo kwenye mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini wa Nyala . Waendesha mashataka waliifahamisha UNAMID kuwa mashtaka dhidi ya Abdelrahman yalitupiliwa mbali baada ya kutopatikana kwa ushahidi.

UNAMID imekuwa ikitaka kuachiliwa huru kwa mfanyikazi wake kwa kuwa ni kinyume na makubalino kati ya UNAMID na serikali ya Sudan. Wafanyikazi wa UNAMID wana kinga , inayowalinda kutokana na mashtaka dhidi yao yanayohusiana na kazi zao.