Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa Mkuu wa UM aweka zingatio juu ya madawa ya kulevya kwenye ziara yake Iran

Afisa Mkuu wa UM aweka zingatio juu ya madawa ya kulevya kwenye ziara yake Iran

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya madawa ya kulevya na vitendo vya kihalifu amewasili nchini Iran ambako atakuwa na majadiliano na wenyeji wake katika maeneo mbalimbali ikiwemo juhudi zinazochukuliwa na nchi hiyo kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya.

Yury Fedotov amesema kuwa ziara yake hiyo ni kama ishara ya kuunga mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Iran kwenye maeneo ya kukabiliana na madawa ya kulevya na maeneo mengine ya kihalifu.Iran inatajwa kuwa mstari wa mbele kwenye vita vya kupiga marafuku usambazwaji wa madawa ya kulevya, na namna inavyoweka zingatio la pekee kwenye tatizo la ugonjwa wa UKIMWI.

Katika ziara yake hii ya siku tatu, mkuu huyu anatazamiwa kukutana na mwenyeji wake rais Mahmoud Ahmadinejad pamoja na maafisa wengine waandamizi. Atatembelea pia eneo moja linalopakana na nchi za Afghanistan na Pakistan