Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka kuwe na mazungumzo kati ya jamii ya Aymara na serikali ya Peru

Mtaalamu wa UM ataka kuwe na mazungumzo kati ya jamii ya Aymara na serikali ya Peru

Mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameishauri serikali ya Peru na viongozi wa makabila ya kiasili Kusini magharibi mwa nchi kufanya mazungumzo ili kumaliza mzozo uliopo kuhusu madini na mafuta. Kulingana na taarifa iliyotolewa na mjumbe huyo ni kuwa karibu watu watano waliuawa na zaidi ya wengine 30 kujeruhiwa mwezi uliopita kwenye mji wa Juliaca kufuatia maandamano ya kupinga uchimbaji wa madini katika eneo hilo .

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa yamii ya Aymara inayoishi kwenye eneo la Puno karibu na mpaka wa Peru na Bolivia imekuwa ikipinga shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo ikidai kuwa mashamba yao yatachafuliwa.