Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama The Hague yamwondosha kamanda wa vita kwenye chumba cha kuzikilizia kesi

Mahakama The Hague yamwondosha kamanda wa vita kwenye chumba cha kuzikilizia kesi

Majaji wanaoendesha kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu inayomkabili kiongozi wa kijeshi wa zamani wakati wa machafuko ya eneo la Balkan, wamelazimishwa kumwondosha mtuhumia huyo kusikiliza kesi hiyo baada ya kitendo chake cha kuwaingilia na kuwakatisha majaji hao wakati wakiendelea na kesi hiyo.

Ratko Mladic anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu uliotendeka wakati wa machafuko ya Yugoslavia alitiwa mbaroni mwezi Mei baada ya kuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 16 ameanza kupanda kizimbani huko The Hague.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo ambaye wakati wa mapigano hayo alikuwa mkuu wa vikosi vya pamoja vya Serbia na Bosnia aliondoshwa toka kwenye chombo kulikoendeshwa kesi hiyo baada ya kupuuzia onyo lilitolewa na jaji mmoja aliyemtaka akae kimya na kuacha maelezo yaliyokuwa yakitolewa na jaji.Pia Jaji Orie alikamribia kamanda huyo kutokana na tabia yake ya kuwasiliana na watu walioketi kwenye ukumbi maalumu wakifuatilia kesi hiyo.