UM wataka kufutiliwa mbali hukumu ya kifo dhidi ya raia wa Mexico kwenye jimbo la Texas nchini Marekani

1 Julai 2011

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea hisia zake kuhusiana na mipango ya kumnyonga Humberto Lael Garcia raia wa Mexico kwenye jimbo la Texas nchini Marekani. Kwa sasa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imemuomba Gavana wa Jimbo la Texas kuibadili hukumu hiyo ili iwe kifungo cha maisha.

Leal alihukumiwa kifo mwaka 2005 kutokana na mashataka ya utekaji nyara, ubakaji na mauaji dhidi ya msichana mmoja wa miaka 16. Wakati huo huo mjumbe maaalum wa Umoja wa Mataifa wa Masuala kuhusu mauaji yaliyo kinyume na sheria Christof Heyns pamoja na mjumbe maalum anayehusika na mateso na vitendo vingine katili au adabu kali Juan Méndez wameiomba serikali ya Marekani kufutilia mbali hukumu hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud