Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO imesikitishwa na Thailand kupinga mkataba wa urithi wa dunia

UNESCO imesikitishwa na Thailand kupinga mkataba wa urithi wa dunia

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ameelezea masikitiko makubwa baada ya tangazo la serikali ya Thailanda kwamba litaupinga mkataba wowote wa kimataifa wenye lengo la kulinda utamaduni wa binadamu uanochukuliwa kama ni urithi wa asili.

Waziri wa serikali ya Thailand amesema mjini Paris ambako kamati ya UNESCO inakutana kwamba nchi yake haiungi mkono mkataba wa UNESCO, hatua ambayo ni ya karibuni kwenye mgogoro unaohusisha hekalu la Preah Vihear, lililo katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO kwamba limeharibiwa wakati wa machafuko kwenye mpaka baina ya Thailand na Cambodia yaliyozuka mapema mwaka huu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)