ICC kumkamata Ghaddafi, mwanae na afisa mwingine wa serikali

27 Juni 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC leo imetoa vibali vitatu vya kukamatwa Rais Muammar Gaddafi, Saif Al-Islam Gaddafi na Abduullah Al-Senissi kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo mauaji.

Uhalifu huo unadaiwa kutekelezwa na vyombo vya serikali yakiwemo majeshi kuanzia Februari 15 hadi Frebeuari 28 mwaka huu wa 2011.

Majaji wa ICC wanasema kuha mazingira yanatosheleza kuamini kwamba washutumiwa hao watatu walitekeleza uhalifu dhidi ya ubinadamu na kukamatwa kwao ni muhimu ili kuhakikisha wanapanda mbele ya mahakama ya ICC, pia katika kuhakikisha kwamba hawaendelei kuingilia na kuhatarisha uchunguzi wa mahakama , na kuwazuia kutumia malaka waliyo nayo kuendeleza uhalifu katika mfumo wa sheria.

Hali ya Libya iliwasilishwa kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka wa ICC na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa azilimio namba 1070 lililopitishwa bila kupingwa tarehe 26 Februari mwaka huu. Fadi El Abdallah ni wa afisa wa masyuala ya sheria ICC.

(SAUTI YA FADI EL ABDALLAH)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter