73,000 wametawanywa ma mapigano Sudan Kusini jimbo la Kordofan:OCHA

23 Juni 2011

Wakazi wa mji wa Kadugli wamekusanyika nje ya ofisi za mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS baada ya kukimbia mapigano. Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanasema bado hayawezi kuwafikia kwa uhuru maelfu ya watu kwenye jimbo la Kusini la Kordofan.

Inakadiriwa kwamba watu 73,000 wametawanywa na machafuko hayo tangu mwanzoni mwa mwezi huu wakati mapigano yalipozuka kati ya majeshi ya Sudan Kusini na Kaskazini.

Watu wengi walikimbilia kwenye ofisi za NMIS lakini wakaondoka na kwenda kutafuta hifadhi pengine Elizabeth Byrs ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter