Balozi mwema ya UNICEF azungumzia umuhimu wa elimu

22 Juni 2011

Mwimbaji mashuhuri duniani na balozi mwema wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa, Shakira amezungumzia umuhimu wa elimu alipokutana na wanafunzi wa kiyahudi na wa kipalestina wanaosoma pamoja kwenye shule moja mjini Jerusalem.

Akiongea alipotembelea taasisi ya Max Payne ambapo kila darasa lina walimu wawili wanaofunza lugha ya kiarabu na kiyahudi, Shakira alisema kuwa ameridhika kama watu wengine kuwa kuwekeza katika elimu ndiyo njia bora ya kuleta amani na utulivu duniani. Tangu ateuliwe kama balozi mwema wa UNICEF mwaka 2003 Shakira amekuwa kwenye mstari wa mbele kwenye programu ya shirika la UNICEF ya kusaidia watoto kujiunga na shule.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter